JE Unafahamu Laana ya Kutembea na Mume wa Mtu na Madhara Yake ?
Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida bila kujua wanajilimbikizia laana itakayofanya maisha yao kuwa magumu mbeleni. Machozi ya uchungu ya mwanamke mwenzio juu ya mume wake hayafutiki haraka.. Ni kama zigo la kinyesi mgongoni linavutiwa na inzi pekeake. Huyo mwanaume unaemuona Leo ana mke, Pesa na mali na kuona ndo fursa kwako kumpata kwasababu anajua kujali na anapesa za kutosha kukugharamia.... Ukirudi nyuma miaka 10-15-20 mwanaume huyo huyo alikuwa kama huyu unae mkataa leo Unaye muona hajui kuvaa.... Hana pesa za kutosha.. Hana mali kwahiyo hakufai. Wanaume wengi wanaanzia chini... Jitihada za wake zao zinawafikisha walipo Leo. Heshimu jitihada hizo. Heshimu siku walizofunga kwa ajili ya waume zao. Heshimu machozi waliomlilia Mungu awafikishe walipo... Heshimu muda na jasho walilolitoa kuhakikisha waume zao wanaonekana watu mbele za watu. Muombe Mungu akupe wa kwako hata kama masikini mpate utajiri pamoja. Na wewe ubige magoti , ulie na...