ZINGATIA YA FUATAYO ILI KUEPUKA MAUMIVU WAKATI WA KUACHANA.
1. Mwamini Mungu maana ni yeye tu asiyebadilika ila Mwanadamu anabadilika. 2. Fahamu kuwa una-date Mtu na sio malaika, anamapungufu na anauhuru wa maamuzi. 3. Kutofaa kwa huyo mpenzi wako haikufanyi kutofaa kwa ulimwengu mzima. Dunia inawatu zaidi ya Billion 7, hivyo akiondoka yeye kuna wenzake Billion 6+ wanakusubiri. 4. Mahusiano sio Ndoa na yameruhusiwa kuvunjika. Hivyo kuachana sio jambo la ajabu wala la aibu. 5. Inawezekana kuvunjika kwa hayo mahusiano ni ishara kuwa Mungu anakuepusha na janga kubwa zaidi huko mbele. Mshukuru Mungu na umwamimi. 6. Samehe, achilia, linda amani ya moyo wako kwani maisha bado yanaendelea. 7. Jipambe, vaa, pendeza, kula vizuri na upate muda wa kupumzika kwani hujafiwa ni kama tu umeacha kazi Kampuni moja kwenda nyingine. 8. Acha kujilaumu kwa yote uliyomfanyia kwani ilikuwa sehemu ya Mchakato wa mahusiano, hata asingekuwa yeye bado ungefanya kwa mwingine. Hakuna sababu ya kuchanganyikiwa. 9. Hatma yako iko mikononi mwa Mungu na ndiye anayeamua kesho y...