Posts

Showing posts from June, 2022

MAPENZI HUWA IMARA PALE YANAPOJENGEWA NJIA YA KUTOKA NA KUINGIA

Image
MPENZI msomaji, naendelea kuelezea ‘topiki’ inayoelezea namna mapenzi yanavyokuwa imara yakijengwa. Tuwe pamoja hadi nitakapoishia. Mwenzi wako atakuheshimu mno kama nawe unamuonesha utiifu. Hata wasaliti wengi, wamejikuta wakisalitiwa baada ya kuwaonesha wenzi wao jinsi wasivyo waaminifu. Onesha utu ili uendelee kufaidi upendo na huduma. Mwenzi wako amekuwa akitumia fedha nyingi kukuhudumia, jambo unalodaiwa kwake ni utu. Hakikisha unampa faraja mpaka hajutii kile anachokitoa kwake. Faraja siyo mapenzi ya kitandani peke yake. Unapaswa kutuliza akili na ujue mwenzi wako anahitaji nini kutoka kwako. Ukishakifahamu, ni juhudi yako kuhakikisha hakikosi. Kufanya hivyo ndiyo utu na ndivyo utakavyoweza kumteka zaidi na zaidi. Atakapokuwa anakutendea lakini maombi yake huyapokei vizuri, unakuwa unamkatisha tamaa. Kadiri unavyomkatisha tamaa ndivyo unavyoelekea kumvunja moyo. Tambua kwamba moyo unapovunjika inakuwa ni ngumu mno kuurejesha kwenye hali yake ya kawaida. Kwa maana hiyo unakuwa ume...

TABIA 30 ZA MWANAMKE ANAYEWEZA KUKUFAA KATIKA MAISHA YAKO

Image
Mwanamke ni mama mwenye nguvu unajua kwa nini kwa sababu mwanamke alitoka katika ubavu wa mwanaume baada ya Mungu kufanya yafuatayo kwa mwanaume A. Alimpa usingizi mwanaume  B. Alimfanyia upasuaji C. Damu ilitoka kwa wingi kwa mawanaume D. Nyama ilitolewa kwa mwanaume  E. Mfupa ulitolewa kwa mwanaume F. Baada ya kufanyiwa hivyo mwanaume ndipo mwanamke akaumbwa akatoka mwanaume akakiri na kusema huyo ni mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu –hivyo ataitwa mwanamke napenda ujue kuwa Mwanamke amebeba uponyaji wa mwanaume na mwanaume amebeba vidonda kwa ajili ya mwanamke Mwanamke ni mfupa mwanaume ni udongo hivyo mwanamke ni: 1. Ni nguvu ya mwanaume 2. Ni jasiri 3. Mchapakazi 4. Mwenye kujiamini 5. Tegemeo la familia  6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla  7. Mlinzi wa mwanaume – Bwana akisema ‘’nimefanya jambo jipya duniani mwamke atamlinda mwanaume  8. Chanzo cha baraka ya familia ( nitabariki Uzao wa tumbo lako) 9. Adui wa maadui wa familia...