Sababu 5 kwanini kila mahusiano mapya unaishia kuachwa!
Unajiona kama mtu mwenye laana, kila ukiingia kwenye mahusiano hayakai muda mrefu, mahusiano yako yanakaa miezi miwili au hata hiyo haifiki unaachwa.unajihisi kuchanganyikiwa, unajiona mbaya, unahisi huwezi kupendwa basi hizi zinaweza kuwa ndiyo sababu unaachwa na si hizo zilizopo kichwani kwako. (1) Unaenda kwa kasi sana kila unapoanzisha mahusiano. Umekutana na mtu, hata hamjajuamna vizuri ushamuambia kila kitu chako, ushaanza kumtambulisha kwa marafiki zako kama mke/mume, ushaanza kutaka kujua kwao, kutaka mfanye vitu pamoja, kuongelea habari za mtoto, unaonyesha mchecheto wa hali ya juu. Kwa mwanaume ukiwa hivi wanawake wenaweza kukupapatikia na kuona uko siriasi ila ukizidisha sana mwanamke mwenye akilia tajiuliza kwanini una haraka, labda kuna kitu unakificha hivyo kurudi nyuma. Kwa mwanamke ukiwa hivi mwanaume anakuona kama umechanganyikiwa sana kuhusu ndoa, anakuona huna maisha na utamsumbua hivyo kukuacha kwani anahisi utakua mzigo kwake. (2) Unalalamika sana kuhusu ma...