*Regeza jicho wakati wa kumtizama mume wako siyo unalikaza mpaka anakuogopa utafikiri uko chooni unakamua kimba lililokataa kuoka * Usiseme nina pua baya sijui nini, mwanamke ukiongea na mumeo hata kama unapua kama nukta nundu shikashika huku ukijifanya kama unamafua vile. Hata kama unasikio kama ungo lipambe kwa hereni siyo lazima za kuning'inia kama mmasai, zipo ndogo akija mume ataliona sikio dogo unakwama wapi mwanamke? Hakuna limbwata zuri kama nywale lakini mmh, kuna baadhi ya watu nywele zimefungwa mabutu wala hazijulikani rangi wala mstari hauonekani. Wanaume wengine wanapenda kuchezea nywele jamani suka vizuri ata twende kilioni , Mume mpaka kula denda anaogopa kwa meno yalivyogandia vinyuzi vya spinachi na maharage Mswaki unaona kama gundi ya viatu, halafu unasumbua watu mume wangu wala hani kiss, mara naombeni jinsi ya kutengeneza limbwata, wakati wewe mwenyewe limbwata hala hujui kujituma Mwanamke una kauli chafu kama choo cha stendi ya ubungo, mume anaona bora arudi ny...