KAMA NDIYO UMEMALIZA CHUO BASI JUA KUA HAKUNA MILIONI 10 ZINAKUSUBIRI MTAANI!
Kama ndiyo umemaliza chuo unatakiwa kujua kua hakuna milioni kumi ambazo zinazurura mtaani na kukusubiri wewe ili uzifanyie biashara. Unatakiwa kujua kua hakuna mzazi ambaye atahangaika kukulipia ada, atakopa na kujinyimka ili usome halafu urudi umuambie nipe na milioni kumi nikafanya biashara na kama wapo ni wachache sana! Kwa wazazi wengi kusoma inaamanisha kuajiriwa na kama utamaliza chuo bila ajira inamaanisha umeshindwa maisha, kwa maana hiyo kama kijana ni lazima ujiongeze wewe mwenyewe, ni lazima uache kusubiri milioni kumi ndiyo ufanye biashara ya kisomi na kuabdilisha hiyo elfu kumi au laki moja ambayo ni rahisi kwako kuipata na kuifanya kuwa milioni kumi. Kama huwezi hivyo basi miaka mitano baadaye utakua umekaa sehemu unalalamika kua ajira hamna na utakutana na watu wengi wa darasa la saba ambao wana biashara zao na ukiwauliza walianza na mitaji kiasi gani watakuambia elfu kumi mpaka laki moja ambayo kwa wakati huo utakua huna au unayo lakini umri nao utakua umeenda....