Posts

Showing posts from May, 2021

KAMA MWANAUME HUMTAKI UNAMBLOCK, NARUDIA UNAMBLOCK NA SI KUMUAMBIA SIKUTAKI!

Image
Kama Mwanaume humtaki basi unamblock na akitumia namba nyingine nayo unaiblock na nyingine nayo unaiblock, meseji zake hujibu bali unazifuta. Lakini kama Mwanaume anakutafuta kila siku unaongea naye unamuambia kuwa humtaki hujamblock huyo Mwanaume anajua kuwa bado unamtaka hivyo ni sitaki nataka. Tena kama uko kwenye mahusiano na Mwanaume wako, kusema nina mtu halafu unapokea simu zake ni kama vile umemkubali, narudia kama una Mwanaume ambaye unampenda na upo kwenye mahusiano au ndoa lakini kuna lijamaa kunakusumbua basi liblock. Narudia, hata kama anatumia namba mia ziblock zote, lakini kusema nimemkataa ila hujamblock mwanaume hatakuelewa. Narudia, mblock, mblock, sijui kama mmenielewa Dada, najua unasema nishamuambia kuwa simtaki, lakini ipo siku atatuma meseji uya hovyo na wanaume hatusamehi kirahisi, najua mblock! NB; Subiri ukishaachwa ndiyo utasema nilishamuambia simtaki, au ndiyo ulalamike inamaana ananiacha kwa sbabau hii?

WADADA AMBAO MLIAHIDIWA NDOA MKIWA CHUONI HEMBU TUPENI UZOEFU WENU!

Image
Mimi ni Binti wa miaka 21, nipo chuo mwaka wa kwanza, naomba ushauri wako, nina mchumba wangu ambaye mwaka huu mwezi uliopita alinivalisha Pete, nampenda na mimi ananipenda, kila kitu tunafanya pamoja na kila mtu anajua kuwa huyu ni mpenzi wangu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, huyu mpenzi wangu ana wivu sana, yaani hataki niwe na mazoea na mwanaume mwingine yoyote, mimi na yeye tunasoma kozi tofauti, kama unavyojua kuwa darasai ni lazima kufanya assignment na tumepangwa magroup ambapo mimi nimepangwa na wakaka wa tatu wadada nao tuko watatu. Sasa kaka hataki kabisa mimi kushiriki nao, ananoapangia muda wa kuonana na kuna Kaka mmoja ambaye ni kama kiongozi hampendi, ameniambia nihakikishe kuwa natafuta group la wanawake tu na kama siwezi ni bora tuachane. Nimemuomba msamaha lakini hataki kunielewa ameniambia kuwa nichague kati ya hilo group au yeye. Nilaimua kuacha kwenda kwenye discussion lakini naona kwenye test nafeli kwani sina mtu wa kusoma naye. nina rafiki wa kike lakini nao ...

Kama unafanya hivi basi jua kuwa unajitengeneze Mateso wewe mwenyewe!

Image
Moja ya vitu ambavyo huwezi kufanya na ukafanikiwa ni kulazimishia mapenzi, hakuna namna unaweza kumlazimisha mtu akakupenda pale anapokuchoka na kwa bahati mbaya jinsi unavyopzidi kumlazimishia mtu kuwa na wewe ndiyo jinsi unavyozidi kumpoteza. Kuna watu kiasilia hawakubali kuachika, hawakubali kuambiwa sikutaki, kwao ni kama dharau, ni kama kusimamisha maisha yao. Kwa wanaume hii inaweza kuwa na unafuu kidogo, kwamba mwanaume unaweza kujilazimishia kwa mwanamke kwa muda mrefu kidogo na mwisho mwanamke akaamua kubaki na wewe. Mwanamke anapokosa mtu mwingine kuna wakati anasema basi bora kubaki na huyu. Lakini kwa mwanamke kujilazimishia kwa mwanaume ni kufungua mlango wa mateso. Iko hivi, ni wanaume wachache sana ambao watakukataa pale ukijilazimishia kwao, kwa mfano, labda mwanaume amekuacha, ana mtu wake, labda kaoa au ni mpenzi wake tu. Kama ukijilizaimishia kwake kwakua unasema unampenda basi huyu mwanaume anaweza asikuache, ataendelea kufanya mapenzi na wewe lakini hatakua mpenzi...

HEKELEA LAKINI SIKU WAKIACHANA HATAKUA NA AMANI MPAKA ADHALILISHE MTU MWINGINE

Image
Katika mahusiano mara nyingi ni nadara sana kukutana na mtu ambaye hajawahi kuwa na mtu. Tena wakati mwingine unaweza kuingia kwenye mahusiano na mtu wa mtu kisha akawa mtu wako. Wakati mwingine hata ukajikuta unaingia kwenye mahusiano na mume au mke wa mtu mkapendana na hata mhusika kumuacha mume au mke wake. Bila kujali sababu zao za kuchana lakini kama unataka kuwa na amani na huyo mtu basi kamwe usifurahie mateso ya mtu mwingine. Kama una mpenzi lakini kila siku akiwa kwako anamuongelea vibaya mpenzi wake wa zamani, anakuambia umpigie simu umtukane, anakuruhusu umtumie meseji za matusi na picha za ajabuajabu ili tu kumuumiza. Anampiga na kumtukana mbele yako huku akikusifia wewe na madudu mengine mengi mengi basi jua kuwa hata ukimpata huyo mtu ipo siku yatakugeukia. Unampenda sawa na pengine huwezi kumuacha lakini acha kufurahia ujinga wake kwakua tu anafanyiwa mwenzako, kumbuka siku huyo mwingine akiondoka basi utafanyiwa wewe huo ujinga. Akikupa namba yake ili umpigia mke/mume w...

MAMBO 5 YA KUYAJUA UNAPOCHEPUKA NA MUME WA MTU AMBAYE ANADAI MKEWE ANAMTESA!

Image
(1) Kugombana si kuachana hivyo hata kama hawapatani namna gani basi jua kuna uwezekano wa kurudiana hivyo usimpe maisha yako yote. Unapoamua kumfanyia vitu kama kumzalia mwanaume huyu, kumpa mtaji kwaajili ya Biashara, kununua kiwanja na kujenga pamoja na mwanaume wa namna hii, kumuamini na kuachana na mpenzi wako kwaajili yake basi jua kuwa unacheza patapotea. Kama hajamuacha mke wake basi bado anampenda. (2) Wanaume wengi wanaoanzisha mahusiano ya nnje ya ndoa kwa kuwashutumu wake zao, kuongelea tabia mbaya za wake zao basi mambo mengi ambayo anakuambia basi ni yeye anayafanya. Inawezekana mwanamke wake akawa ni mkorofi lakini ni kwakua amechoka tabia zake, wanaume wengi wanaonyanyaswa na wake zao hawasemi kwani huona aibu, wao hupenda kujisifia kua wao ndiyo hutesa ila ukweli ndiyo huteseka, ukisikia anajisifia kuteseka basi kua makini mara mia. (3) Kama ameoa kwa maana kafunga ndoa na huyo mwanamke hata kama anakupenda namna gani na anakushirikisha kwa kila kitu lakini kisheria ye...

CHEKELEA LAKINI SIKU WAKIACHANA HATAKUA NA AMANI MPAKA ADHALILISHE MTU MWINGINE

Image
  Katika mahusiano mara nyingi ni nadara sana kukutana na mtu ambaye hajawahi kuwa na mtu. Tena wakati mwingine unaweza kuingia kwenye mahusiano na mtu wa mtu kisha akawa mtu wako. Wakati mwingine hata ukajikuta unaingia kwenye mahusiano na mume au mke wa mtu mkapendana na hata mhusika kumuacha mume au mke wake. Bila kujali sababu zao za kuchana lakini kama unataka kuwa na amani na huyo mtu basi kamwe usifurahie mateso ya mtu mwingine. Kama una mpenzi lakini kila siku akiwa kwako anamuongelea vibaya mpenzi wake wa zamani, anakuambia umpigie simu umtukane, anakuruhusu umtumie meseji za matusi na picha za ajabuajabu ili tu kumuumiza. Anampiga na kumtukana mbele yako huku akikusifia wewe na madudu mengine mengi mengi basi jua kuwa hata ukimpata huyo mtu ipo siku yatakugeukia. Unampenda sawa na pengine huwezi kumuacha lakini acha kufurahia ujinga wake kwakua tu anafanyiwa mwenzako, kumbuka siku huyo mwingine akiondoka basi utafanyiwa wewe huo ujinga. Akikupa namba yake ili umpigia mke/...

MWANAMKE USIFURAHIE KUTONGOZWA UKAJIONA UNAPENDWA BALI FURAHIA KUWA TAYARI UNAE UMPENDAYE

Image
Kuna faida kubwa kwa Mtu kuwa na mtu UMPENDAYE kuliko kuwa na mtu AKUPENDAYE ila wewe humpendi kwa sababu furaha na amani halisi inaanza na UTASHI wako mwenyewe Wengi tunajikuta njia panda kwa sababu ya kutaka kujua UPENDO WA MWINGINE KWAKO huku ukisahau kwamba:- UNAWEZA KUPENDWA NA MTU KWA SABABU ZAKE NA USIJUE JAPO KUNA UNAYO FURAHIA UKIAMINI NI UPENDO . Utashi ni mapokeo ya MOYO baada ya uhitaji wa NAFSI na hapo ndipo UPENDO hujengwa, ndo Maana hata ninasema ANZA WEWE KUPENDA Kabla ya KUPENDWA kwani Kuna faida, Maana ukimpenda mtu tafuta KUAMINIWA KATIKA UPENDO Ndipo utaona MAPENZI YANAVYO WEZA KUJITENGENEZA MENYEWE japo ni jambo linalohitaji Muda mpaka kufikia FURAHA NA AMANI YAKO Uwiano wa UPENDO haujawahi onekana, Ila kilicho kuwepo katika MAPENZI ni kukubari kwamba NAWEZA KUJENGA IMANI YA MWINGINE KUONA NAMPENDA ndipo iwe rahisi wewe kupendwa, Mfano hai :- MWANAMKE ANAWEZA KUWA NA MAWASILIANO NA MWANAUME ILA YEYE KAMA YEYE HAJAJENGA WAZO LA MAPENZI ILA MWANAUME ALIOMBA MAWASI...

MAHUSIANO NA NDOA NYINGI ZA SASA NI SAWA NA NGUO ILOCHAKAA KUTWA UPO KWA FUNDI KUZIBA VIRAKA🤦‍♂️

Image
Wengi wanatafsiri MAHUSIANO AMA NDOA kama hakika ya kuwa na mtu kwa ajili ya kukamilisha MAHITAJI iwe ki mwili ama ki maisha, badala ya maana halisi kwamba;- UNAPOINGIA UHUSIANO AU NDOA UNAWAJIBIKA KUMPENDA MWENZA WAKO KAMA UNAVYOJIPENDA MWENYEWE. Ubinafsi umekuwa kipaumbele kwa jamii yetu kiasi kwamba kila mmoja anataka apewe nafasi kubwa kuliko mwingine. Ili upendwe na kupewa thamani kwenye MAPENZI unawajibika kugharamia iwe kwa MALI AU MWILI Migogoro imekuwa chakula cha mahusiano na ndoa nyingi kuliko UPENDO hata kupelekea maumivu makubwa kwa kila aliyeamini katika UPENDO Kwa sasa ili japo upate FURAHA NA AMANI ya mpito unatakiwa kujipima uwezo wako ki fedha ili wewe utoe pesa na mwingine akupe haja yako Maana kumpata mtu sahihi ambaye atakuwa nawe kwa MOYO wake unawajibika kuomba rehema za MUNGU ili kumpata huyo, Kwa nadharia ni kama ndo FASHION lakini kumbe MAJERAHA YA MAPENZI YAMEWAJENGA WENGI KUAMINI HAKUNA UPENDO WA DHATI Japo najua kabisa MAPENZI YA KWELI BADO YAPO ila tu ku...