UNAJUA KWAMBA MAISHA YA KUIGIZA YAMETAWALA KWENYE MAHUSIANI MENGI YA SIKU HIZI

Maisha ya kuigiza yanatubeba na kutawala mahusiano ya sasa.
Kila mtu hautaki ukweli wa maisha.
Ukiwa mkweli unaonekana ndo mwongo na wale waongo ndo wanaonekana wa kweli.
Mwisho wa siku majuto huanza sababu uliujua ukweli lakini ukajifanya kufumba macho usione, kuziba masikio usisikie na ukajifanya pia umejitoa ufahamu na akili ikakataa kuelewa kumbe unaelewa.

Ni bora ukamkubali anayesema ukweli na kuishi maisha ya ukweli na uhalisia.
Japo wengi tunahukumiana kwa mapungufu yetu ila lazima tujue hakuna binadamu aliye mkamilifu.
Angalia mapungufu ya mwenza wako nae ajue yako ili mjue kama mtaweza kuishi hivyo hivyo au hamtowezana.
Hapo sasa kila mtu atafanya uamuzi wa busara ili huku mbeleni msije laumiana.
Ukweli uwe mwanzoni.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KURIDHISHANA WAKATI MWANAMKE AKIWA KWENYE HEDHI

ZIJUE TABIA HIZI ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA.

UNADHANI NI MWANAMKE YUPI AMBAYE ANATESEKA ZAIDI HAPA