UNAJUA KWANINI KUNA NDOA AMBAZO ZINADUMU KWA MUDA MREFU.




 


Ukiona watu wanaendelea kuishi pamoja kama mume na mke kwa muda mrefu basi jua kuwa wamevumilia mengi. Ndo sio jambo la mchezo ndugu yangu. Kuna watu walikuwa kwenye ndoa lakini yalivo washinda wakatoka leo hii hawana hamu tena ya ndoa

🥲. Usiikimbilie ndoa kama hujajiandaa kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.
Omba sana MUNGU akupe mtu atakaeweza kuyabeba mapungufu na madhahifu yako.🙏
NDOA NYING ZIMEKUFA
Kilicho baki ni kusogeza tu siku
Usishangae kusikia mke na mume kuna wakat wanaweza wasisemeshane kwa siku nzima au zaidi.. Na wana kula na kulala pamoja... Kuna wengine utakuta ni miez sasa imepita bila kupeana haki yao.
Basi ni kudra MUNGU zinazo hitajika kumnusuru anae fanya au kufanyiwa hayo.Mtu ambae ana teseka na ndoa yake amechoka mpaka kutaman ivunjike kesho lakin anapo waza juu ya mali walizo tafuta pamoja na malezi ya watoto
Basi mke au mume ana amua kuendelea kuumia ili kulea familia
Kuna wakat unaish na mtu lakini mambo anayo kufanyia hayavumiliki...ni zaidi ya uchafu au dharau kwani ana utesa moyo na hisia zako kadri anavyo taka..ndugu na jamaa wamejaribu kusuruhisha lakin imeshindikana
KULAZIMISHA UPENDO
KUJITESA NA KUUMIA
umri wako bado huenda una kupa nafas kupata mpenz atakae weza kufaa hata kama sio leo ila kesho utapata.bora uwe SINGLE kuliko UPENDO wenye kukutesa....
Hata hivyo kuwa na watoto ktk NDOA haimanishi kuwa lazima ufe ukiwa ndan ya NDOA...
wakat mwingine unapo jitunza mwenzako huko ana zunguka na kukuletea magonjwa ndani....
..UNAE MPENDA HAKUPENDI ni jambo la kawaida ktk mapenz ko vyema kuangalia unapo pendwa maana kesho waweza pata moyo wa kurudisha upendo kwake huyo anae kupenda kuliko kulilia sehem usiyo pendwa.
FAHAMU FAIDA ZA KUOA MWANAMKE MCHA MUNGU
1 Maombi ya mwanamke yaweza kufungua familia toka kwenye vifungo vya Ibilisi
2 Maombi ya mwanamke yaweza kufungua mpaka kizazi cha nne.
3 Maombi ya mwanamke yaweza kuhuisha upya nafsi na roho hata palipokatika tamaa.
4. Maombi ya mwanamke ni ulinzi wa familia yako
5. Maombi ya mwanamke yaweza kuwa ni patanisho la familia
6. Maombi yamwanamke ni toba kwa familia
7. Maombi ya mwanamke ni baraka na mafanikio ya familia
8. Maombi ya mwanamke ni ngao imara katika familia
9. Maombi ya mwanamke yaleta faraja ya familia
10. Maombi ya mwanamke yaondoa laana za kurithi
Mwanamke, usichoke kuomba maana nyie ndio walinzi wa familia zenu na tena vita vyenu ni vya roho kwa hiyo yawapasa kupigana vita katika ulimwengu wa roho na si ulimwengu wa mwili. "Kesheni mkiomba"
Tuma ujumbe huu kwa kila mwanamke unayempenda na kutaka awe na maisha mazuri na familia yenye furaha na MUNGU atakubariki,
Nakupenda sana mke wangu❤️
💕JINSI YA KUISHI NA MKEO💕
●Usimfokee mke wako unapozungumza. Inamuuma sana. ( Mithali 15:1 )
● Usiseme mabaya juu yake kwa mtu yeyote. ( Mwa. 2:19 )
●Usishiriki mapenzi yake na mwanamke mwingine. Unaitwa Uzinzi. ( Mt. 5:28 )
●Usimlinganishe mke wako na mwanamke mwingine. Ikiwa yule mwanamke mwingine alikuwa mwema kwako, Mungu angekupa wewe. ( 2 Kor. 10:12 )
●Usimruhusu kamwe akusihi ngono. Anamiliki mwili wako kama unavyomiliki mwili wake.
( 1 Kor. 7:5 )
●Kuwa mpole na mwenye kukubalika. Amejitolea sana kuwa na wewe. Inamuumiza sana wakati wewe ni hash na inakera. Kuwa mpole. ( Efe. 4:2 )
●Usimfiche chochote.
Sasa wewe ni mmoja na yeye ndiye msaidizi wako.
Acha kusiwe na siri unayomficha.
( Mwa. 2:25 )
●Usitoe maoni mabaya kuhusu mwili wake. Alihatarisha maisha na uzuri wake kubeba watoto wako.
Yeye ni nafsi hai si nyama na damu tu.
●Usiruhusu mwili wake uamue thamani yake. Mthamini na umthamini hata uzeeni.
[ Efe. 5:29 )
●Usimzomee hadharani na faraghani.
Ikiwa una tatizo la kutatua naye, lifanye ukiwa katika faragha ya chumba chako.
( Mt. 1:19 )
●Mshukuru na umthamini kwa kukutunza wewe, watoto na nyumba yako vizuri. Ni dhabihu kubwa anayofanya.
( 1 The 5:18 )
●Wanawake wote hawawezi kupika kwa njia ile ile; thamini chakula cha mkeo.
Si rahisi kupika milo mitatu kwa siku, siku 365 kwa mwaka kwa miaka kadhaa. ( Met. 31:14 )
●Usiwaweke ndugu zako mbele ukamsahau yeye huyo ni mke wako.
{Yeye ni wewe na wewe ni yeye}.
Lazima aje mbele ya familia yako. ( Mwa. 2:24 )
●Tumia muda pamoja naye kufanya funzo la Biblia na kusali. ( Yakobo 5:16 )
●Tenga wakati wa kucheza naye na kufurahia ushirika wake.
Kumbuka wakati umekufa, atakuwa karibu na kaburi lako lakini marafiki zako wanaweza kuwa na shughuli nyingi na kushidwa kuhudhuria mazishi yako.
( Mhubiri 9:9 )
●Usitumie pesa kamwe kumdanganya au kumdhibiti.
Pesa zako zote ni zake.
Yeye ni mrithi pamoja nawe wa neema ya Mungu. ( 1 Pet. 3:7 )
●Usionyeshe udhaifu wake.
Kuwa ngao karibu naye. ( Efe. 5:30 )
●Waheshimu wazazi wake na kuwa mwema kwa ndugu zake.
●Usiache kumwambia jinsi unavyompenda siku zote za maisha yake.
Wanawake hawachoki kusikia hivyo. ( Efe. 5:25 )
●Kuwa kama Mkristo, Hiyo ndiyo njia pekee unayoweza kuwa mume mwema na mcha Mungu. ( Rum. 8:29 )

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KURIDHISHANA WAKATI MWANAMKE AKIWA KWENYE HEDHI

ZIJUE TABIA HIZI ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA.

UNADHANI NI MWANAMKE YUPI AMBAYE ANATESEKA ZAIDI HAPA