Unaweza kuwa kwenye mahusiano yaliyokufa zamani ila ukawa kama mtumbwi uliotelekezwa majini ukisubiri wimbi liupige usogee ufukweni.


Upo kwenye mahusiano mawasiliano shida, umuanze wewe, hata ukipewa nafasi yeye ni kuitikia tu nakusikia, ongea, oooooh mara mimi sina neno.

Unaweza kuwa kwenye penzi lilikufa ambalo ukiomba kitu ndio chanzo cha ugomvi na kususiana ili tu ujiongeze.

Unaweza kuwa kwenye mahusiano yaliyofika mwisho usipoomba kuonana naye hata mwaka hawezi kukuambia muonane lasivyo siku amekosa kitu huko kwingine ndipo akukumbuke kwa ajili ya hitaji lake na baada ya hapo kila mtu afanye yake.

Unaweza kuwa kwenye mahusiano yaliyokufa kila leo unaambiwa na wewe ni mwanaume au mwanamke sasa unavyojiona ila wewe unahisi ni utani (kuna ukweli katika neno natania au katika utani)

Unaweza kuwa katika mahusiano yaliyokoma ila ukabakizwa kwasababu una mshahara, biashara, unasaidia mambo yake yaende, mmejenga au mna watoto.

Mnaweza kuwa katika mahusiano yaliyokufa ila wazazi ndio wanayashikilia muwe pamoja ingawa si kwa umoja yaani mnaishi kwa sababu wazazi wanataka au kwasababu ya heshima yake kanisani au kwenye jamii.

Kuna mahusiano au ndoa zishakufa ila zinalindwa na kitu kidogo sana ambacho kinamteketeza mmoja ila mwingine anafurahia maisha.

Ujumbe huu ni wako msomaji ...
@maisha_halisitz
Natamani ujue namna ya kunitumia nikusaidie vitu vingi mno
Karibu kwenye huduma zangu za ushauri na group la wachumba nichek WhatsApp no 0656832100

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KURIDHISHANA WAKATI MWANAMKE AKIWA KWENYE HEDHI

ZIJUE TABIA HIZI ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA.

UNADHANI NI MWANAMKE YUPI AMBAYE ANATESEKA ZAIDI HAPA