Yako wapi yale mapenzi aliyokuahidi?
Uko wapi ule uaminifu aliokuhakikishia? Iko wapi ile furaha ya vitendo pamoja na amani ya moyo aliyokuwa anaizungumzia kila iitwapo leo? Havipo tena eeh!!!? Upo wewe kama wewe na sasa hivi unamwona kama mnyama huyo ambae alikuja akiwa mwema na akidai hana kasoro yoyote.
Ukamwamini na kumkubali na bila kusita ukamkabidhi moyo wako, mwili pamoja na maisha kiujumla. Leo hii mapenzi yamepotea na dhoruba imeingia kwenye maisha yako. Majuto ndo usiseme hadi unajuta kuyajua mapenzi.
Kila siku umekuwa wa kutoa machozi na maisha yako yamekuwa ya sintofahamu na hujui nini cha kufanya bali umebaki njia panda tuu.
Mpendwa! Mahusiano yasiendelee kukukosesha maana ya maisha, lazima maisha yako yaendelee. Kwani kabla yeye kuja kwenye maisha yako ulikuwa hupumui? Ulikuwa huli ukashiba? Ulikuwa hupati usingizi? Ulikuwa huvai ukapendeze? Ya nini, ya nini, ya nini wewe, kubali kuachia.
Ifikie hatua uthamini sana utu na muda wako kuliko kuendea kuumia kwa kubembeleza penzi la mtu asuejua thamani yako na anekupitisha kila siku kwenye milima na mabonde bila kuifikia furaha.
Kumbuka: Maisha yako ni bora sana kuliko kumng'ang'ania mtu uliekutananae ukubwani. Ishi Maisha yako huku ukiendelea kumuaomba Mungu akuletee mtu bora.
Comments
Post a Comment