𝐀𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐒𝐈𝐑𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄



😠😠😠😠
🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎
1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere! Ndio aridhike.
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!
4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!
🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹
5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye! Muda huo upo hospital
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao!
🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓
7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote!
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!
🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓
9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika! Hawa ni wengi mno
10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!
🍠🍠🍠🍠🍠🍠🍠
11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka wanaharisha!
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
13. Wako ambao wakishikwa na Hasira wao ni Simu na wao kutwa zima sebuleni pressure IPO juu kama nyoka wa kijani ole wako umwondolee simu utajuta kuzaliwa haswa wana sumu kama Kali mno ila Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.😂😂😂
🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓
14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.
15.Yuko ambaye ukimkasirisha hasira zote atatamani kukuonesha mapenzi ya dhati yaani hakuna kuondoka nyumbani kila Mara anakuangalia na kukuchokoza kazi hazifanyiki siku hiyo ni kufuata mashariti tu.
🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀
16. Yuko akikasirika Hataki mlale chumba kimoja ataenda kulala chumba kingine au mzungu wa NNE.
🙄🙄🙄🙄🙄🙄
17.Yuko akikasirika ni matusi mwanzo mwisho yaani kiufupi nyumba haikaliki omba usiwe uswazi coz kijiji cha watu watasikia
😠😠😠
18.Yuko akikasirika Huzoa mabegi kutishia anarudi kwao ila wanaume tulio na akili hatukupembelezi utatoa mabegi na kuyarudisha ndani mwenyewe.Nawaibia kasiri kidogo wanaume wenzangu Mwanamke wa namna hii Mara nyingi hupenda kubembelezwa kama mtoto wengi wao wamekulia kwa Bibi/ Babu / shangazi au kwa mjomba .
💕 💕 💕 💕 💕 💕 💕
19.Mwanamke mwingine akikasirika utasikia anapiga simu kwa shoga ake waende picnc ole wako umzuie utakula mateke kama ya vandame.
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
20. Mwanamke mwingine akikasirika huitaji zawadi yeye ili kutuliza akili yake wewe njoo na zawadi yoyote anayoipenda atatulia.
🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼🌼
21.Mwanamke mwingine akikasirika anaweza kujifanya amepandisha majini kumbe vyote hivyo ni vitisho tu hasira ikishuka analainika kama bamia za soko la Kilombero
🧞‍♀🧞‍♀🧞‍♀
22.Mwingine akikasirika yeye atachukua kitabu cha nyimbo za Tenzi za Rohoni, Kaswida, music, kuangalia sinema, kusoma Riwaya Mafunzo ya Joh angalizo kwa wanaume Mwanamke wa namna hii kama ameshika rimoti mwache usimguse unaweza kuchezea mbata za uso.
🤜🏻🤜🏻🤜🏻
23.Mwingine akikasirika hasira zake zitaishia kwenye bar angalizo Mwanamke wa namna hii ni rahisi kukusaliti hivyo akitaka pombe ni bora anywe akiwa nyumbani🍻🍻🍻 hata hivyo pombe sio suluhu ya hasira.
24.Mwanamke mwingine akikasirika ni mwendo wa kugonganisha meno kama ngiri aliyejeruhiwa na mkuki wa hivi Mara nyingi huwa wana macho makubwa, unakuta jicho limetoka pima kama Ndulele za Simiyu🤥🤥🤥
25.Mwanamke mwingine akikasirika hasira zake atazimalizia bafuni ole wako uwe na sinki utamkuta amelala ndani ya maji huku kichwa kipo nje, Kama ni maji tiririka atanunua boza siku hiyo na ogopa kama mmepanga mabafu au vyoo vya uswahilini foleni itawahusu siku hiyo.
🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎🍎
26.Mwanamke anayekupenda kwa dhati ameoza kakuelewa tepetepe kwako kidume akikasirika yaaani Hutaenda kazini atakutazama kama sinema la posta raha yake akuone wewe akikuruhusu kwenda kazini sio simu zitakazopigwa xku hiyo ole wako usipokee.
🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟
27.Kuna Mwanamke mwingine akikasirika hutaka kuonesha umwamba kwa mwanaume atafunga kanga kiunoni anakuita njoo nje tupigane ukimwagalia kiganjani hajai mdogo kama piritoni wengi wao huwa wana kazi zao hivyo hufanya hivyo ilihali akijua mume wake sio mtu wa ngumi ( kutest mitambo )� Mkurya, Wazaramo, Wakwere na Mnyiramba (Nkue ndante Mintanda)
hizi kabila mungu anawaona japo na Mimi nimo humo kazi yng ni kusema ukweli.😤😤😤🐰🐰🐰🐰🐰🐰🐰🐰🐰🐰🐰
28.Hasira zingine humfanya Mwanamke alime sana kama ni MTU wa shamba asome sana kama ni mtu wa masomo kuloweka miguu kwenye beseni kama ni mwanachuo ili mradi umemkasirisha.
💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜💜
29.Ataiba kama ni penzi kujaribu na yeye ili mradi umemkosea kama ni wadukani funga kibanda siku hiyo atakuibia bila kujua anajiibia mwenyewe hujisemea "Huyu mbwa Leo atakoma" yote hiyo n hasira tu hawa viumbe ni shida.
🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓🍓
30.Mwanamke mwingine akikasirika hapati tabu atapiga magoti kuutafuta USO wa mungu ulipo akiona imani ndogo xku hiyo ataenda kanisani au msikitini akiona amekosa hivyo atamtafuta kiongozi wa Dini Mchungaji au Shekh ataeleza kilichomkasirisha mwanzo hadi mwisho aina ya wanawake hawa sio waongo atalia mbele ya mtumishi wa Mungu ataombewa na kurudi nyumbani kwa Furaha kuikumbatia familia yake na kusahau yote mkono wa mungu sio mfupi utaiponya familia 👨‍👩‍👧👨‍👩‍👧👨‍👩‍👧
💕 Daktari wa Mahaba

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KURIDHISHANA WAKATI MWANAMKE AKIWA KWENYE HEDHI

ZIJUE TABIA HIZI ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA.

UNADHANI NI MWANAMKE YUPI AMBAYE ANATESEKA ZAIDI HAPA