DADA MPENDWA, USHAURI BORA WA MAHUSIANO KWAKO🌹🌹
1. Tafadhali usimuonyeshe mwanaume kuwa unampenda sana, usimjulishe kuwa huwezi kufanya kitu chochote bila
yeye. Atakuchukulia poa, kukusaliti au kufanya chochote anachotaka kwa sababu anajua unampenda sana.
2. Usilie, usikate tamaa au kufa kwa sababu ya mpenzi wako. kwanini ulie au unywe sumu kwa sababu amekuvunja moyo? Hakuwahi kukupenda huyo.
3. Kama mwanamke, jipe heshima, lazima umuonyeshe mwanaume wako ajue kwamba unaweza kuishi bila pesa zake. Usiombe muda wa maongezi, pesa za nywele au nguo kutoka kwake. Tafuta chanzo cha mapato naye atakuheshimu.
4. Acha kudhibitisha kuwa wewe ni mzuri kwenye ngono na uchumba tu, sio mzuri kwenye ndoa. Wanaume huwa wanakuwa wenye akili na busara linapokuja suala la kuchagua mwenzi wa ndoa.
5. Usijisikie kana kwamba ulimwengu unakaribia mwisho kipindi mwanaume ameamua kuondoka kwako. Usimsihi abaki, wewe ni wa thamani sana kuomba hilo dada yangu. Atakutendea na kukuona kama takataka.
7. Usijaribu kujilazimisha kumpenda mwanaume, ni sawa na kumfundisha nguruwe jinsi ya kuthamini uzuri na usafi alionao.
Msimlazimishe mwache aende zake.
8. Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kumsihi mtu akupende. Upendo huja automatic
9. Usihuzunike kamwe kama mpenzi wako anampenda mwanamke mwingine kuliko wewe. Haimaanishi kuwa kuna kitu kibaya kwako. Inamaanisha tu kwamba hukukusudiwa kuwa wako....
.
🍏Daktari wa Mahaba🍏
Comments
Post a Comment