FUNZO KWA WACHEPUKAJI!
Mwanamke mmoja alichukua Simu ya mumewe na kuingia kwenye Facebook yake.
Alitambua na kuona mazungumzo ya kimapenzi anayofanya na wanawake.
Alikaa chini na kufikiria njia ambayo anaweza kutumia kwa urahisi kumtenganisha na wanawake.
Alikuja na wazo zuri, bila hata mume kujua. Alikuja na mbinu zifuatazo.
Alinakili mazungumzo yake yote na mmoja wa wanawake hao (screenshot).
Alifungua akaunti mpya ya Facebook yenye jina la Mwanaume.
Alituma ombi la urafiki kwa mume, na alikubali ombi hilo bila kujua ni mke wake.
Baada ya kukubali ombi. Walianza kuchat na yeye akaficha utambulisho wake na kujitambulisha kwake kwa namna nyingine.
Alisema, "Mimi ni Abu Dar'daee ndio jina langu, Mwanachama wa AL SHABAB. Niliona mazungumzo yako yote na mke wangu. Kwa hiyo nataka kutumia njia hii kukuonya ujiepushe naye kama kweli unataka kuendelea kuishi. Ili kuondoa shaka yoyote kwako, nina mazungumzo yote na ni haya hapa, unaweza kuona.
Kwa hivyo, kama hutaacha kuzungumza na mke wangu basi nitakuchinja kama kondoo.
Nakujua. Nakujua kweli. Jina lako ni Jamilu baba yako anaitwa Mohammed, mama yako anaitwa Khadija, una watoto 3. Al'amiyn, Zahara na Yusuf.
Abdulrahman ni rafiki yako mkubwa na Usman ni jirani yako. Wewe ni Mhadhiri wa chuo kikuu. Pia unaenda kazini saa 3:30 asubuhi na rafiki yako Usman, unamfuata Luchelele..
Ninakuonya kama utathubutu kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kuzungumza na mke wangu tena, nitakuchinja kama Kondoo kama nilivyosema awali."
Mke alikuwa karibu naye wakati anasoma ujumbe huo. Alipokuwa anasoma, alikuwa akitetemeka na kurudia "Innalillahi WA innaillaihirraji'un".
Alimuuliza nini kimetokea, hakusema chochote. Mara moja akafuta Facebook na Whatsapp yake na mitandao mingine yoyote ya kijamii.
Kesho yake asubuhi alienda kuuza simu na kununua vyakula vya nyumbani...🙆😂
🍏Daktari wa Mahaba🍏

Comments
Post a Comment