UTOFAUTI WA MTU ANAYEKUJALI NA ASIYEKUJALI.


.
- Anaye kujali atakupa kipaumbele... Mfano: hata kama yuko na message mia, yuko radhi achelewe kujibu za wengine ili ajibu yako kwanza.
.
* Asiye kujali kwake huna nafasi, kila siku utakua chaguo la mwisho kwake au la kwanza pale anapokosa wa kuwa nae.
.
- Anaye kujali anakukumbuka, neno "Busy" huwa halina nafasi kwake kwaajili yako. Hata akiwa busy vipi lazima atatenga muda kukuzungumza/kuonana na wewe.
.
*Asiye kujali hata akiwa hayuko busy anaweza jifanya yuko busy ilimradi tu apate sababu ya kuwa mbali na wewe, na kuwa karibu na wengine.
.
- Anaye kujali anakuhurumia, akigundua una tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi, mfano kuumwa, iwe umemwambia/hujamwambia, lazima atafanya vyovyote vile ilimradi atoe msaada.
.
* Asiyejali huwa hanaga huruma, unaweza ukamwambia shida zako na akawa na uwezo wa kuzitatua lakini asikusaidie, akawa na uzito ndani yake.
.
- Anaye kujali huwa na tabia ya kuwa mfatiliaji wa lolote utakalo mwambia. Mfano: Baby najisikia kichwa kinauma. Lazima baadae utaona anakutafuta ''Baby unaendeleaje? Kichwa kimepoa?".
.
*Asiyekujali huwa sio mfatiliaji, tena mkiagana ndo imetoka hiyo. Ukikausha, usipokumbushia na yeye wala hana mpango nayo.
.
- Anayekujali anapenda kuwa wa kwanza, mfano: Unapoamka utakuta kashatext, anapiga, birthday yako utakuta kakuwish kwenye wale watu 5 wa mwanzo.
.
*Asiyekujali huwa anapenda kuwa wa mwisho, kila siku hupenda kuanzwa yeye. Salamu, maongezi, message, simu, nakadhalika hupenda kuwa wa mwisho, yani wewe uanze na yeye ndo amalize. Hawa ndo wazuri kwenye kujibu "Love u too, miss u too".
.
- Anayekujali ni ngumu kusahau, ukiona mtu anasahau mara kwa mara birthday yako, ahadi alizo kuahidi, ulichomuomba, yani tabia hizo zikiwa zinajirudia mara kwa mara basi ujue kuna tatizo hapo maana anayekujali huwa anakuweka akilini.
.
*Asiyekujali huwa ni msahaulifu sana wa vitu muhimu kutoka kwako, yani unaweza ukawa kila siku unamkumbushia kitu kimoja halafu baadae kasahau.
.
- Anayekujali huwa anapenda kukujudge kuendana na mood yako, unaweza ukamwambia "Niko poa baby", lakin akakutazama akakuambia "Usijali, najua hauko poa", au ukamtusi halafu baadae ukaomba msamaha ukasikia "Usijali, nilikuona una hasira ndomana sikukujibu".
.
*Asiyejali yeye hanaga huo muda wa kukusoma mood, ukimjibu hovyo atakuchapa vibao, akikuuliza 'una njaa??" Ukajibu "Hapana" ndo basi tena hiyo.
.
- Anayekujali hujenga tabia ya kufanya chake chako, shida zako zake, anapenda kukuona una furaha, akikufanyia jambo huwa hasubirii kulipwa au kupewa shukrani japo huwa anatamani asikie mdomo wako ukimsifia, anapenda kukuelekeza kuliko kukukomoa pale unapokosea, anapojua hujui kitu basi atakuelimisha mpaka uelewe, ni muelewa sana unapomwambia kitu, mwepesi wa kushukuru, mwepesi wa kuomba msamaha, anajali muda, kila kitu hufanya kwa hiari.
.
- Asiyejali huwa chake chake chako chake, shida zako ni zako tu, uwe na furaha usiwe nayo wala hana mpango, akikufanyia kitu anataka kulipwa au utasikia "Khaaa hata kushukuru", anapenda sana kukomoana kuliko kuelekezana pale unapokosea, akigundua hujui kitu flani inakua ndo kama sababu ya kukucheka na kukudharau, mgumu wa kukuelewa mpaka umpe sababu kibao, "ASANTE" linakuja kwa misimu kama mvua, mgumu kuomba msamaha, hajali muda "Ukimuita, atakuja kwa kujivuta na kujiradhimisha", kila kitu kufanya hadi m-bembelezane.
.
Hayo ni baadhi, yapo mengi sana na mifano ipo mingi sana ila niishie hapa.
I hope sasa utakuwa umeelewa.
.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KURIDHISHANA WAKATI MWANAMKE AKIWA KWENYE HEDHI

ZIJUE TABIA HIZI ZA MSICHANA ANAYEPENDA LAKINI HAWEZI KUSEMA.

UNADHANI NI MWANAMKE YUPI AMBAYE ANATESEKA ZAIDI HAPA